Ifahamu Monaco, moja ya nchi tajiri duniani

Ifahamu Monaco, moja ya nchi tajiri duniani

 Ifahamu Monaco, moja ya nchi tajiri duniani


Moja ya nchi tajiri zaidi duniani ni Monaco. Inajulikana kwa kuwa na idadi kubwa ya mabilionea ingawa ni nchi ndogo Barani Ulaya. Inapatikana kando ya Ufaransa na Bahari ya Mediterranean. Licha ya udogo wake Monaco imejaa matajiri wengi huku watu wakiipachika jina la ‘Maskani ya Mabilionea’.

Ukikatiza katika barabara za Monaco ni kama kuna maonesho ya magari, kwani hakuna gari za kawaida na badala yake utakutana na gari za kifahari kama Mercedes Benz, BMW, Rolls Royce, Bentley, Ferrari na Lamborghini. Vilevile magari hayo hutumika pia kama Tax kwa watalii.


Idadi ya watu wanaoishi Monaco ni takribani 38,000 na wengi wakiwa mabilionea ambao wamekimbia nchi zao kwa ajili ya kufuata usalama katika nchi hiyo. Monaco haitegemei miradi ya mafuta ama gesi kuingizia mapato na badala yake hujiingizia mapato kupitia watalii, Yacht, Monte-Carlo Casino, hoteli za kifahari, maduka ya brand za juu pamoja na Formula One – Monaco Grand Prix (mchezo wa mashindano ya magari) mashindano hayo yanatajwa kupata mamilioni ya pesa kila mwaka.

Kuhusu usalama ni wa hali ya juu katika nchi hiyo hakuna wizi kamera zipo kila kona na polisi wapo kila mahali. Watu wanaweza kutembea na vito vya thamani bila kukumbana na vishandu na hii ndio sababu inayowafanya matajiri kukimbilia katika nchi hiyo.

Inasemekana kuwa hadi watoto wa miaka 5 wanamiliki magari ya kifahari kama Rolls-Royce si kwa kuendesha wenyewe bali hupewa kama zawadi na wazazi wao ikionesha ishara kuwa nchi yenye utajiri zaidi. Ikumbukwe katika nchi hii hakuna kodi ya mapato inayokatwa kwa wananchi

Post a Comment

0 Comments