Unapenda kunukia ijue historia ya Perfume

Unapenda kunukia ijue historia ya Perfume

 Unapenda kunukia ijue historia ya Perfume

Kati ya vitu ambavyo baadhi ya watu hutumia pesa nyingi kuvinunua ni manukato ‘Perfume’. Lakini je unafahamu historia yake?

Kabla ya jina la ‘Perfume’ kutumika manukato hayo yalipewa majina tofauti katika nchi mbalimbali ambapo Misri ya kale manukano yalikuwa yakiitwa ‘Kyphi’ au ‘Shemen’. Kwa upande wa Wagiriki walitumia jina la ‘Mýron’, Waarabu waliita ‘Itr’ au ‘Attar’.

Aidha kwa watu wa Roma wao walitumia majina kama ‘Unguentum’ au ‘Perfuma’ ambapo hapo ndipo lilipopatikana jina linalotumika sasa la ‘Perfume’ ambalo linatokana na neno la kilatini ‘Per Fumum’ neno hilo likiwa na maana ya ‘Kwa Mvuke’.



Kabla ya viwanda kushika kasi kutengeneza manukano, zamani yalikuwa yakitengenezwa kwa njia asili. Ambapo watu walikuwa wakikusanya maua kama waridi, jasmine na violets, kisha kuyaweka katika mafuta ya mimea au ya wanyama kwa muda na baada ya hapo kuyapika ili harufu iliyopo kwenye maua iweze kuingia katika mafuta na kupata perfume.

Nchi ya kwanza kutumia na kutengeneza perfume ilikuwa Misri ya kale ambapo Wafalme na mapriest walikuwa wakivutiwa zaidi na harufu nzuri kutokana na kuwaletea heshima, utukufu na hadhi ambapo walitumia katika sehemu mbalimbali ikiwemo katika sherehe za kidini pamoja na mazishi ya kifalme.

Baada ya Misri, Wagiriki na Waroma walichukua sanaa hiyo wakitumia katika sehemu mbalimbali. Mara baada ya kusambaa katika nchi hizo mbili sanaa na ubunifu huo ulipenya kwa Waarabu ambapo kwa upande wao waliamua kuboresha baadhi ya vitu. Wao wakitengeneza perfurme kwa kutumia mchanganyiko wa mimeo, viungo na mkaa wa asili kutengeneza harufu za kipekee.

Aidha watu waliona fursa katika manukato, hivyo basi biashara ya perfume ilienea Ulaya, Mji wa Grasse huku Ufaransa, ikawa kitovu cha perfume, na mpaka ilipofikia karne ya 17 na 18, perfume ilipata umaarufu mkubwa, na hadi sasa imekuwa biashara kubwa duniani huku baadhi zikiuzwa hadi dola milioni 1.5.

Post a Comment

0 Comments