Kama unadhani ili upendeze ni lazima uvae mavazi ya gharama basi unajidanganya. Hili limewekwa wazi na Miss Grands Tanzania 2025, Beatrice Alex ambaye pia aliiwakilisha nchi katika mashindano ya Miss Grand International 2025 yaliyofanyika nchini Thailand na kuibuka nafasi ya 6 (5th Runner-Up), kati ya washiriki kutoka nchi 77 duniani.
Beatrice wakati akizungumza na Mwananchi alipokuwa anapatiwa ubalozi wa kampuni ya kubashiri ya Bang Bet ametoa siri ya mtu kupendeza hata kama akivaa nguo za bei ya chini.
"Mimi navaa nguo hata za Sh45000. Kwa sasa najaribu kuunda brand yangu lakini sitaki kuamini kwamba hapa nimevaa milioni tano. Unaweza ukavaa kwa bei nafuu ukaenda Ilala ukapata nguo nzuri. Kupendeza haiendani na bei, jijue, fahamu aina ya mwili wako na rangi gani zinakukaa vizuri,"anasema.
Anasema kila hatua aliyokuwa akienda katika mashindano ya Miss Grand yalikuwa yanampa funzo.
"Nidhamu, jiamini na kuna baadhi ya vitu utaambiwa ni vigumu kutimiza. Lakini niamini kwamba, wewe mwenyewe ndiyo unajua kuwa unaweza na fanya hadi uwashangaze watu.
"Changamoto ambazo nimewahi kukutana nazi ni kutamani kufikia matamanio ya watu. Nilikuwa na presha natamani kufanya vitu vikubwa hadi ambavyo vipo nje ya uwezo wangu,"anasema.
Kuhusu baadhi ya familia za Kiafrika kupuuza vipaji vya watoto wao Grace anasema familia yake imekuwa ikimpa ushirikiano wa kutosha.
"Tangu niliposhiriki Miss Tanzania 2022 nilikuwa chuo. Lakini niliomba ruhusa nyumbani walikuwa wananisapoti kwa ambacho walikuwa nacho, hata sasa niliwaambia wakaonesha ushirikiano kikubwa nisiwavunjia heshima tu," anasema.

0 Comments