CNN ni wimbo wa hip-hop wa rapa marehemu Albert Mangwea 'Ngwair' na Fid Q uliyoachiwa rasmi mwaka 2009 ukiwa kama moja ya ngoma inayopatikana kwenye albamu ya Ngwair inayofahamika kama (N'GE 1982), ambayo pia ilitoka 2009 ikisheheni ngoma nyingine kama Birthday N'ge.
Wimbo wa CCN ulirekodiwa katika studio za Bongo Record chini ya mtayarishaji nguli wa muziki nchini ambaye pia ni mmiliki wa studio hiyo, P Funk Majani mwaka 2009.
Wimbo huo uliitwa CCN baada ya wanamuziki hao kufananisha mtindo wao wa maisha na washikaji zake wakukesha bila kulala kutokana na kula bata (Starehe) na kazi zao za muziki ambazo zilizochukua usingizi wao. Hivyo wakatengeneza wimbo ukielezea wanakesha muda wote kama chombo cha habari Duniani cha CNN.
Awali Fid Q hakutakiwa kuwepo kwenye wimbo huo na msanii aliyetakiwa kuhusika ni Babu wa Kitaa 'Saiduuu'. Ambaye ni mtangazaji lakini pia kaka wa msanii Country Wizzy. Lakini kulingana na ratiba kuwa ngumu hawakuweza kurekodi ndio akaingia Fid Q.
Kwa mujibu wa Fid Q anakwambia ile verse yake inayosikika kwenye wimbo wa CNN ni ya pili ambayo alibadilisha baada ya kusikia verse ya marehemu Ngwair na kuona ilivyo kali zaidi. "Usiniite half men niite men and Half".
Fid Q ambaye ni msanii nguli wa hip hop anayeaminika anakwambia katika historia yake ya muziki Ngwair ndio msanii pekee amewahi kumfutisha verse na haijawahi tokea tena. Nadhani unaelewa kwanini Ngwair alikuwa tishio kwa rapa wengi.
CNN ambayo video yake imesheheni mastaa kibao wa tasnia Bongo, mpaka sasa unatajwa kama moja kati ya wimbo Classic za muda wote kuwahi kutokea katika historia ya muziki wa Bongo Fleva

0 Comments