Huko nchini Korea Kusini kuna shindano maarufu lijulikanalo kama ‘Space Out Contest’ ambalo washiriki wanatakiwa kukaa kimya bila kufanya shughuli yoyote kwa muda wa dakika 90.
Ili uweze kushinda na kuondoka na zawadi basi unatakiwa kufuata masharti ambapo mshiriki yoyote hatoruhusiwa kuongea, kutumia simu, kulala au kufanya shughuli yoyote na badala yake anatakiwa kutulia, kutazama anga, au kuwa kimya bila kuonesha huzuni.
Mshindi wa Space Out Contest hapati fedha kama ilivyo katika mashindano mengine. Badala yake hupatiwa cheti, tuzo, na zawadi ndogo kama bidhaa, kifurushi cha spa au programu za meditation.

Aidha inaelezwa kuwa lengo kuu la shindano hilo linatajwa kuwa ni kuhamasisha watu kupunguza msongo wa mawazo unaotokana na maisha ya kila siku. Waandaaji wanasema mashindano haya yanatoa nafasi kwa watu kupumua, kupunguza shinikizo, na kurejesha utulivu wa ndani, kipindi ambacho wengi wamezidiwa na kazi, mitandao ya kijamii na presha za maisha ya kila siku.
Mbali na Korea Kusini zipo nchi nyingine ambazo zimewahi kujaribu kufanya shindano hilo ikiwemo China, Uholanzi, Marekani, Canada, na maeneo mbalimbali barani Ulaya. Zikitumia shindano hilo kusaidia watu tatizo la Afya ya akili.

0 Comments