Bwana harusi alivyoingiza mkwanja kupitia suti ya harusi

Bwana harusi alivyoingiza mkwanja kupitia suti ya harusi

 Bwana harusi alivyoingiza mkwanja kupitia suti ya harusi


Wakati vijana wengi wakihangaika kutafuta hela za kufanikisha harusi zao, jamaa mmoja kutoka Ufaransa aitwaye Dagobert Renouf, alikuja na mbinu ya kufanya matangazo kupitia suti ya harusi iliyomuingizia mkwanja mrefu.

Akiwa hana kitu mfukoni huku akifikiria kuachana na kuoa Renouf alipata wazo la kutumia suti yake ya harusi kama ‘Bango la Matangazo’ kwa kuweka logo za makampuni makubwa.

Aliingia mtandaoni na kutangaza nafasi kwenye suti yake kama ambavyo timu za mpira zinavyoweka matangazo kwenye jezi, cha kushangaza kampuni zaidi ya 26 zilivutiwa na wazo hilo na kuanza kulipia nafasi hizo.



Kila kampuni ililipia kulingana na sehemu waliyotaka logo yao ikae, sehemu zinazonekana kwa haraka zilikuwa zililipa gharama kubwa na ndani ya muda mfupi Renouf alikusanya zaidi ya euro 10,000, kiasi kilichomsaidia kumalizia maandalizi ya harusi huku akibaki na okoto la kuanzia maisha.

Siku ya harusi suti yake ya rangi ya kijani ilikuwa na logo ndogo za makampuni yaliyolipia fedha tukio ambalo liliibua hisia kwa wageni waalikwa huku wengi wakimpongeza kwa ubunifu huo na wengine wakimpatia jina la ‘Marketing Genius’.

Post a Comment

0 Comments