YANGA YACHAPWA 3-2 NA KMC MECHI YA KIRAFIKI GYMKHANA

YANGA YACHAPWA 3-2 NA KMC MECHI YA KIRAFIKI GYMKHANA

 

TIMU ya Yanga SC imechapwa mabao 3-2 na KMC FC katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam.
Mabao ya KMC yamefungwa na Daruwesh Saliboko mawili na beki Nickson Joseph Mosha moja, wakati ya Yanga yamefungwa na viungo na Mkongo Maxi Mpia Nzengeli na Mguinea, Balla Moussa Conte.
Mchezo huo Ulikuwa sehemu ya maandalizi ya Yanga ya mchezo wake wa kwanza wa Kund B Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS FAR Rabat ya Morocco Jumamosi ya Novemba 22 Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments