SERENGETI BOYS YAITANDIKA SUDAN 6-0 KUFUZU AFCON U17

SERENGETI BOYS YAITANDIKA SUDAN 6-0 KUFUZU AFCON U17

 

TANZANIA imeibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Sudan Uwanja wa Kimataifa wa Dire Dawa mjini Dire Dawa nchini Ethiopia katika mchezo wa Kundi B michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya CECAFA.
Mabao ya Tanzania ‘Serengeti Boys’ katika michuano hiyo ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON U17) yamefungwa na Dismus Athanas dakika ya 10 na 16, Nhingo Luzelenga dakika ya 21, Kassim Juma dakika ya 57, Soann Shaaban dakika ya 74 na Hamisi Baruani dakika ya 80.
Mchezo nyingine mbili za Kundi A michuano ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati — wenyeji, Ethiopia wameifunga Rwanda 2-0i, wakati Somalia imetoka sare ya 2-2 na Sudan Kusini.

Post a Comment

0 Comments