
KIKOSI cha Yanga SC kimeondoka mapema leo kwenda Zanzibar kwa matayarisho ya ‘mwisho mwisho’ ya mchezo wake wa kwanza wa Kund B Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS FAR Rabat ya Morocco Jumamosi ya Novemba 22 Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Ikumbukwe Jumamosi Yanga ilichapwa mabao 3-2 na KMC FC katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam – mabao ya KMC yakifungwa na Daruwesh Saliboko mawili na beki Nickson Joseph Mosha moja, wakati ya Yanga yalifungwa na viungo na Mkongo Maxi Mpia Nzengeli na Mguinea, Balla Moussa Conte.
0 Comments