Umewahi kujiuliza kwanini pete ya ndoa huvaliwa mkono wa kushoto katika kidole cha nne ? Jibu ni hili asili yake inatokana na imani za kale, hasa kutoka kwa Warumi na Wamisri wa zamani.
Wamisri waliamini kuwa ndani ya kidole hicho cha mkono wa kushoto kuna mshipa unaoitwa vena amoris. Wengine huuita mshipa wa upendo, kwani unatoka katika kidole hicho unaoenda moja kwa moja hadi kwenye moyo wa binadamu.
Kwao, kuvaa pete kwenye kidole hicho kulimaanisha moyo wa mume na mke umeunganishwa na upendo wa kudumu moyoni. Warumi baadaye walirithi imani hiyo na kuifanya sehemu ya mila zao za ndoa, jambo lililoenea hadi Ulaya na baadaye duniani kote.
Hata hivyo kwenye baadhi ya tamaduni, kama Urusi na India, pete ya ndoa huvaliwa mkono wa kulia. Lakini maana yake hubaki ile ile kiapo cha uaminifu wa milele. Kwa ujumla, kuvaa pete ya ndoa kwenye kidole cha pili cha mkono wa kushoto ni ishara ya heshima, mapendo, na unaounganisha wanandoa hata wanapokuwa mbali kimwili.

0 Comments