
Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa zamani wa klabu za Simba SC na Yanga SC
, Senzo Mbatha Mazingiza
, ametangazwa kuwa Mtendaji Mkuu mpya wa klabu ya TRA United FC
.
Senzo, ambaye ana uzoefu mkubwa katika uongozi wa soka barani Afrika, amewahi kufanya kazi na vilabu vikubwa kama Yanga na Simba SC, ambako alisaidia kuimarisha miundombinu ya kiutawala na mafanikio ya ndani na kimataifa.
Ujio wake ndani ya TRA United unatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika usimamizi wa klabu hiyo, hususa katika upande wa utawala na uendeshaji, huku lengo likiwa ni kuijenga timu hiyo kuwa miongoni mwa vilabu vinavyoshindana vikali kwenye ligi kuu ya NBC.
Karibu tena Tanzania Senzo Mbatha!
0 Comments