Baada ya Ukame wa Magoli, Dube Aahidi Moto Mkali Yanga

Baada ya Ukame wa Magoli, Dube Aahidi Moto Mkali Yanga

 

Mshambuliaji wa Yanga SC, Prince Dube, ameweka wazi kuwa hana mpango wa kukaa kimya tena, akiahidi kurejea kwenye ubora wake na hata kuvunja rekodi aliyoweka akiwa Azam FC.

Dube, ambaye kwa sasa amekuwa akipitia kipindi kigumu kutokana na kushuka kwa kiwango chake, amesema anajua mashabiki wanahitaji makali yake yale ya zamani na amejipanga kuhakikisha anarudi kwa nguvu mpya.

“Najua wananikumbuka nikiwa Azam, nilifunga magoli zaidi ya 10 kwa msimu mmoja. Huu msimu nataka kuivunja hiyo rekodi na kuisaidia Yanga kupata mafanikio zaidi,” alisema Dube kwa kujiamini.

Mshambuliaji huyo raia wa Zimbabwe ameongeza kuwa amekuwa akifanya kazi kwa bidii mazoezini na anaamini muda si mrefu mashabiki wataanza kuona matokeo.

Kwa sasa, benchi la ufundi la Yanga linaendelea kumwamini Dube, likiamini kwamba kurejea kwake kwenye kiwango bora kutakuwa silaha muhimu katika harakati za timu kutetea ubingwa wa ligi.

Post a Comment

0 Comments