Katika maisha ya ndoa ya mwanasoka wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Ronaldo De Lima tunagusia mmoja wa watoto wake wa kiume ambaye ameamua kuachana na masuala ya soka na kuwa DJ wa muziki. Twende pamoja!
Kati ya watoto wanne wa Ronaldo de Lima (49), ni mmoja tu, Ronald (25) ndiye alionyesha nia ya kufuata nyayo za baba yake katika soka, lakini baadaye akaamua kuwa DJ, kazi anayoifanya hadi sasa.

Katika hili unaweza kusema Ronaldo ni kama kasalitiwa na wanawe,kwani watoto wake wengine watatu wamechagua kufanya vitu vingine nje ya soka. Kwa leo, tutamtazama kiundani Ronald ambaye ni mtoto wa kwanza wa Ronaldo aliyempata katika ndoa yake ya kwanza na mwanasoka, Milene Domingues ambaye ndoa yao ilidumu kwa miaka minne.
Ronaldo, mshambuliaji wa zamani wa Inter Milan na Real Madrid, akiwa katika kilele cha mafanikio yake, mnamo 1999, alifunga ndoa na Milene ambaye kwa sasa ni mchambuzi maarufu wa michezo nchini Brazil.
Kufikia Aprili 6, 2000, huko Milan nchini Italia, wakajaliwa mtoto wao wa kwanza waliyempa jina la Ronald ambalo linatofautiana kidogo sana na la baba yake mzazi. Mama yake Ronald, Milene, pia alikuwa mchezaji akiichezea timu ya taifa ya Brazil mara 20 na kuvunja rekodi ya dunia ya Guinness kwa kupiga danadana zaidi ya 55,000 bila kuangusha mpira akiwa na umri wa miaka 17.

Kuwa na wazazi wenye vipaji hivyo, wengi walidhani Ronald angekuja kuwa mchezaji mkubwa wa soka duniani na kuweka rekodi mbalimbali kama wazazi wake lakini haikuwa hivyo. Badala yake, Ronald aliamua kuwa DJ, akitumia jina lake kama utambulisho wake. Inasemekana baba yake, ambaye ni mpenzi mkubwa wa muziki, alimtia moyo pindi alipochagua kazi hiyo.
DJ Ronald amejiweka kisasa zaidi kwa kuweka mixing za muziki wake mtandaoni ambazo zimepata mamilioni ya wasikilizaji kwenye Spotify, huku akijizolea wafuasi zaidi 431,000 katika ukurasa wake wa Instagram.
Moja ya mafanikio yake makubwa ni kutumbuiza mbele ya mashabiki 60,000 wa klabu ya Cruzeiro ambayo Ronaldo aliichezea 1993/94, na sasa anaimiliki baada ya kununua sehemu kubwa ya hisa zake.
DJ Ronald alipiga muziki kabla ya mechi ya timu hiyo dhidi ya Vasco da Gama mnamo 2022, mechi iliyowapa Cruzeiro nafasi ya kupanda daraja kwenye Brazilian Serie A, huku baba yake akimtazama kutokea jukwaani.
Kwa sasa Ronald ni mmoja wa maDJ wanaoheshimika sana huko Ibiza, kisiwa cha Hispania kinachosifika kwa muziki wa dansi duniani.
Ingawa amechagua kupita njia tofauti kabisa na ile ya baba yake, bado Ronaldo anaonyesha kujivunia uamuzi wa kijana wake huyo hata akiwa na 'malejendi' wenzake kama David Beckham.
Akizungumza kupitia Instagram Live mnamo 2020, Ronaldo alimueleza Beckham kwamba mwanae ameamua kuwa DJ maana mara nyingi alimuona akisikiliza muziki.
"Yeye ni DJ mzuri sana na kwa sasa yuko Brazil. Yeye kuwa DJ, kwa upande fulani naweza kusema ni kosa langu maana nilikuwa nacheza CD kila wakati nyumbani," anasema Ronaldo na kuongeza:
"Hivyo alikuwa akiniona nikisikiliza muziki mwingi, na hatimaye akaamua kuwa DJ. Anafanya vizuri sana, anapiga muziki hata mtandaoni. Watu nchini Brazil na kila mahali wanampenda."
Mwaka uliopita, DJ Ronald alicheza muziki katika klabu tatu tofauti huko Ibiza, akithibitisha kuwa muziki umempa nafasi ya kipekee katika ulimwengu wa burudani. Hata hivyo, katika utoto wake Ronald alipenda soka na kulicheza akionyesha dalili za kufuata nyayo za wazazi wake. Mathalani mwaka 2017, aliitwa kwenye kikosi cha Brazil cha vijana chini ya umri wa miaka 18.
Taarifa hiyo hiyo ilikuja siku chache tu baada ya George Weah Jr., mtoto wa aliyekuwa Rais wa Liberia na gwiji wa soka, George Weah, kusaini mkataba na Paris Saint-Germain (PSG).
Ronaldo akiwa na furaha kubwa aliposti picha Instagram ya kikosi hicho cha Brazil ambacho alikuwepo mwanaye, akionyesha kujivunia hatua hiyo.
"Hii ndio timu ya Brazil kwa ajili ya mashindano ya Maccabiah. Nimeipokea kwa kipekee hatua ya mwanangu Ronald Lima ambaye yuko kwenye kikosi hiki cha vijana. Kila la heri, twende tukashinde," alieleza.

Ila licha ya hatua hii, Ronald alionekana kuwa na mlima mrefu sana wa kupanda ili kufikia mafanikio ya baba yake, na ndilo wengi walikuwa wanataka kuona kipi atafanya. Ikumbukwe Ronaldo De Lima akiwa na wa umri wa miaka 17, tayari alikuwa bingwa wa dunia, baada ya kuwa sehemu ya kikosi cha Brazil kilichoshinda Kombe la Dunia 1994 nchini Marekani.
Mwaka 1996, alijiunga na Barcelona akitokea PSV kwa ada ya Pauni 13 milioni, na kuwa mchezaji ghali zaidi duniani wakati huo. Mwaka uliofuata, alivunja rekodi tena alipohamia Inter Milan kwa Pauni 19 milioni, kisha kushinda tuzo ya Ballon d’Or.
Alishinda tena Ballon d’Or mwaka 2002, baada ya kuibuka Mfungaji Bora kwenye Kombe la Dunia la mwaka huo, ambapo Brazil ilitwaa ubingwa.
Na baadaye alijiunga na Real Madrid kwa Pauni 33 milioni, ambapo alishinda La Liga katika msimu wake wa kwanza. Pengine mafanikio na rekodi za Ronaldo, Mchezaji Bora wa FIFA mara mbili, kwa sehemu yalimtisha hata mwanaye Ronald. Kwa mazingira kama haya, na mengine ndani na nje uwanja, unadhani Ronald angefanya nini zaidi ya kuwa DJ?

0 Comments