Kwa wakati fulani, Watayarishaji wa Muziki (Producers) hutia vionjo vya sauti zao kwenye baadhi ya nyimbo ili kuleta ladha itakayotoa burudani ya uhakika kwa wapenzi wa muziki. Hata hivyo, utaratibu huo umekuwa sawa na kuchovya asali kwa mara ya kwanza.
Hiyo ni kwa sababu katika Bongo Fleva, baadhi ya watayarishaji hujikuta wakiangukia katika uimbaji mara baada ya kufanya hivyo. Baddest 47 na Nahreel, ambaye pia ni msanii wa kundi la Navy Kenzo, ni miongoni mwa waliopita njia hiyo.
Nahreel
Kabla ya kuanzishwa kwa kundi la Navy Kenzo au Pah One alipoanza, Nahreel alikuwa akitambulika zaidi kama mtayarishaji wa muziki. Kazi hiyo aliipenda tangu akiwa kijana mdogo sana, na hii ilichangiwa na baba yake mzazi pale alipomnunulia kinanda.
Katika utayarishaji wa muziki, amepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kushinda tuzo ya muziki Tanzania (TMA) 2015 kama Mtayarishaji Bora. Pia ameweza kufanya kazi na wasanii wakubwa pamoja na kampuni mbalimbali za matangazo.
Nahreel, akiwa kama mwimbaji ndani ya kundi la Navy Kenzo, walipata mafanikio makubwa zaidi walipoachia wimbo wao, Kamatia (2016) uliowaweka sehemu nyingine kabisa kimuziki, na ukiwa ni wimbo wao wa kwanza kutazamwa mara milioni 1 YouTube.
Pia uliwawezesha kushinda tuzo ya WatsUp TV Africa Music Video 2016 nchini Ghana kwenye kipengele cha Best African Group/Duo Video. Hadi kufikia hapo, utaona kwamba baada ya Nahreel kukubali kuimba, aliamua kubaki humo humo.
Na hadi sasa Navy Kenzo wakiwa wametoa albamu tatu ambazo ni AIM (Above Inna Minute) (2016), Story Of The African Mob (2020) na Most People Want This (2023).
Baddest 47
Kwa upande wake Baddest 47, alipata umaarufu baada ya kutoa wimbo wake, Nikagongee (2019), uliopendwa wengi hasa vijana kutokana na kile kilichoimbwa ndani yake starehe na pombe.
Wimbo huu aliurekodi mwenyewe asubuhi akiwa Kyela mkoani Mbeya na hakuamini kama ungeweza kuja mkubwa kiasi cha kumtambulisha.

Hivyo, Baddest 47 naye pia kabla ya kuanza kuimba alikuwa Mtayarishaji wa Muziki tangu mwaka 2011 akijulikana kama Pizo Tachez. Kutoa wimbo huo na kufanya vizuri, naye ameamua kubaki kama mwimbaji.
Hili linatokea kutokana na kwamba mara kadhaa watayarishaji wamekuwa wakilalamika kuwa hawapati kile wanachostahili kutokana na kazi zao.
Hadi kufikia sasa, Baddest 47 ni miongoni mwa wasanii waliofanya vizuri zaidi kwenye Bongofleva katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, huku akishinda tuzo kadhaa za TMA.
Lakini ikumbukwe Baddest 47 na Nahreel, niliyemtaja hapo awali, sio watayarishaji pekee Bongo walioimba na kufanikisha kazi zao. Miongoni mwao ni Man Water na S2kizzy.
Man Water
Ni mshindi wa TMA 2013, anafanya kazi zake studio za Combination Sound. Man Water anakumbukwa na wengi kwa kumfanya 20 Percent kuwa msanii mkubwa hadi kushinda tuzo tano za TMA 2015 kwa mpigo.
Ni mkali wa kuingiza sauti za chini (back vocal), huwa hakosei katika hili, alishafanya hivyo katika nyimbo kama ‘Dushelele’ wa Alikiba, 'Yahaya' wa Lady Jaydee, pia amesikika vizuri katika wimbo wa Mr. Blue, Nipende Kama Nilivyo (2012).
S2kizzy
Tangu akiwa Switch Records hadi alipofanikiwa kumiliki studio yake, Pluto Repulic, S2kizzy amesikika katika nyimbo nyingi za wasanii mbalimbali na kufanya vizuri, huku yeye akiwa bado ni mtayarishaji mkuu.
S2kizzy ambaye ni mshindi wa TMA 2021, sauti yake ipo katika wimbo wa Diamond Platnumz, Kanyaga (2019) ingawa hajatajwa kushiriki kama msanii.
Pia sauti yake imesika katika nyimbo kama; Pochi Nene wa Rayvanny, Wanaona Haya, Dogoli za Country Boy, Turn Me On wa Whozu, Alewa ya Lulu Diva, Hesabu wa Nikki wa Pili, Gibela wa Chino Kidd, Swing wa OMG (Young Lunya, Conboi na Salmin Swaggz) na kadhalika.

0 Comments