Mwamba Huyu Yupo FITI Tayari Kuitumikia SIMBA

Mwamba Huyu Yupo FITI Tayari Kuitumikia SIMBA

 images-72.jpeg

Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally, amethibitisha rasmi kuwa Mohamed Bajaber sasa yuko fiti asilimia 100 baada ya kurejea vizuri kutoka majeraha yaliyomuweka nje kwa muda.

Bajaber tayari alianza kuonekana uwanjani kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya JKT, akicheza dakika 30 na kuonyesha kiwango kizuri, huku Simba ikipata ushindi mnono wa 6-0.

Ahmed Ally amesisitiza kuwa mchezaji huyo sasa yuko tayari kikamilifu kuisaidia timu kwenye mechi zinazofuata, akisema wanasimba wajipange kuona kile wanachokikosa kwa muda mrefu — ubora na ubunifu wa Bajaber katikati ya kiwanja.

Wanasimba mpo tayari kuona moto wa Bajaber ukirudi dimbani?

Post a Comment

0 Comments