SIMBA NA YANGA MECHI ZOTE MWAKANI MACHI 1 NA MEI 3 MKAPA

SIMBA NA YANGA MECHI ZOTE MWAKANI MACHI 1 NA MEI 3 MKAPA

 

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetoa ratiba mpya ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara inayohusisha meci zilizoahirishwa – mwezi Oktoba ambazo sasa zitachezwa Desemba.
Mechi hizo ni Tanzania Prisons na mabingwa watetezi, Yanga SC Desemba 2 kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, TRA United dhidi ya Simba SC itakayochezwa Desemba 3 kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora na Azam FC dhidi ya Singida Black Stars kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Aidha, mechi ya watani wa jadi, ya kwanza itachezwa Machi 1 mwakani, Yanga wakiwa wenyeji nay a pili Mei 3 Simba wamkiwa wenyeji – zote zikipigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuanzia Saa 11:00 jioni.

Azam na Yanga itapangiwa siku, Yanga na Azam itachezwa Mei 19 Uwanja wa KMC Complex, Mwenge,Dar es Salaam – wakati Simba na Azam ni Desemba 6 Uwanja wa Mkapa na Azam na Simba itapangiwa tarehe.
Mechi ya marudiano ya mahasimu wa Jiji la Mbeya, Tanzania Prisons na Mbeya City itachezwa Machi 18 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Post a Comment

0 Comments