Ali Kamwe “Waarabu Watajuta Kupangwa Kundi Moja na Yanga, Wachague Wakutusindikiza Robo Fainali”

Ali Kamwe “Waarabu Watajuta Kupangwa Kundi Moja na Yanga, Wachague Wakutusindikiza Robo Fainali”

 images-79.jpeg

“Nataka nikuhakikishie ndugu, hawa waarabu uliowataja watajichagua mmoja wa kwenda na sisi Yanga hatua ya Robo fainali, kama ni kutoka Morocco, Algeria au Misri lazima watajichagua mmoja wapo atusindikize hatua ya Robo fainali ya mabingwa barani Afrika”

“Msione naongea hivi sisi Yanga tupo serious kuliko ninyi mnavyofikiri, kwaiyo lazima wajichague tupate mmoja wao tuende nae Robo fainali “

Afisa habari za klabu ya Yanga Ally Shaaban Kamwe amesema klabu ya Yanga itaanza safari kesho Novemba 18 majira ya Saa tatu asubuh kuelekea Zanzibar kwaajili ya maandalizi ya mechi dhidi ya Far Rabat.

Ameyasema hayo akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kwanza wa makundi ya Ligi ya Mabingwa ikiwa ni safar ya kwenda kujiandaa kuwakabili Far Rabat ya Morocco.

Aidha Kamwe amesema katika safari hiyo watakosekana baadhi ya wachezaji ambao bado wapo kwenye majukumu ya Timu ya Taifa ambao ni Dube,Ecua na lassine Kouma ambao wameandaliwa utaratibu wa kuungana na timu Moja kwa Moja huko zanzibar.

🗣 Ally Kamwe

Post a Comment

0 Comments