Mahakama yawataka wanaoigiza wapenzi Tiktok kufunga ndoa

Mahakama yawataka wanaoigiza wapenzi Tiktok kufunga ndoa

 Mahakama yawataka wanaoigiza wapenzi Tiktok kufunga ndoa

Mahakama yawataka wanaoigiza wapenzi Tiktok kufunga ndoa

Mahakama kutoka wilaya ya Kano nchini Nigeria imewaamuru watengeneza maudhui ya mapenzi katika mtandao wa TikTok Idris Mai Wushirya na Basira Yar Guda, kufunga ndoa ndani ya siku 60.

Wawili hao walijikuta mikononi mwa sheria baada ya video zao za kimahaba kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, hasa TikTok, zikionyesha wakibusiana na kuonesha mapenzi hadharani jambo ambalo limechukuliwa kama kukosa heshima kwa mila na dini katika jimbo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mahakama hiyo video hizo zilikiuka maadili ya jamii, na hivyo kuamua njia bora ni wawili hao ni kufunga ndoa rasmi. Mahakama pia imeiomba Bodi ya Hisbah kusaidia maandalizi ya harusi hiyo.

Aidha inaelezwa kuwa upande wa wazazi wa Idris wamesharidhia ombi hilo lakini kwa upande wa familia ya Basira inasemekana bado inaendelea na majadiliano ya kina, hata hivyo kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vianadai kuwa wawili hao watakapo kubaliana kuoana watakabidhiwa nyumba ya kuishi na Serikali.

Kesi hiyo imezua mjadala mkubwa nchini Nigeria, wengi wakijiuliza kama ni sahihi kwa mahakama kumlazimisha mtu kuolewa au kuoa kwa sababu ya video ya mtandaoni. Lakini licha ya maandalizi ya harusi kuanza ndoa hiyo itafanyika tu endapo Idris na Basira watakapokubali kwa hiari yao wenyewe mahakama hiyo ikisema kuwa haitamlazimisha yoyote kuoa/kuolewa bila idhini yake.

Post a Comment

0 Comments