Kwa mara nyingine wasanii wa Tanzania watemwa Grammy

Kwa mara nyingine wasanii wa Tanzania watemwa Grammy

 Kwa mara nyingine wasanii wa Tanzania watemwa Grammy

Waandaaji wa tuzo kubwa zaidi duniani katika sekta ya muziki Grammy wameachia orodha ya wasanii watakao wania tuzo hizo huku mastaa wa Bongo Fleva wakitemwa kwa mara nyingine katika kinyang’anyiro hicho.


Kwa mujibu wa orodha ya uteuzi iliyotangazwa na ‘The Recording Academy’, vipengele vinavyohusu muziki wa Afrika vimeendelea kutawaliwa na mastaa kutoka Nigeria kama Burna Boy, Rema na Tyla kutoka Afrika Kusini.

Aidha msanii aliyeongoza kupata uteuzi mwingi zaidi ni Burna Boy ambaye ameteuliwa kuwania vipengele vitatu akifuatiwa na Rema viwili, Tyla viwili huku Davido akiateuliwa katika kipengele kimoja cha ‘Best African Music Performance’

Utakumbuka kuwa nguli wa muziki wa Hip-Hop nchini, Fareed Kubanda maarufu Fid Q na Ambwene Yessayah (AY) waliandika historia mpya baada ya kuingizwa katika mchujo wa Tuzo za Grammy.

Ambapo kwa upande wa Fid wimbo wake wa ‘Glory 2’ aliomshirikisha Damian Soul na Jose Chameleone ndio uliofanikisha hilo huku upande wa AY wimbo ‘Anganeka’ akiwa na Kanjiba na ule ‘Simuoni’ aliofanya na Harmonize ukiwa umemuingia kwenye mchujo huo.

Mbali na wasanii hao naye mkali wa Bongo Fleva, Harmonize nyimbo zake nne zilifanikiwa kuingia katika hatua hiyo ya mchujo wa kuwania tuzo za Grammy, nyimbo hizo ambazo ni ‘Me Too’ ft Abigail Chams, ‘Simuoni’ aliyoshirikishwa na Ay, ‘Furaha’, na ‘Finally’ aliyomshirikisha Miri Ben-Ari, ambazo ziliwasilishwa katika kipengele cha ‘Best African Music Perfomance’.

Tuzo hizo za 68th za Grammy zinatarajiwa kutolewa Februari 1, 2026 nchini Marekani.

Post a Comment

0 Comments