Filamu itakayoelezea maisha ya marehemu mfalme wa Pop kutoka Marekani Michael Jackson ‘MJ’ rasmi inatarajiwa kutoka Aprili 24,2026.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye ukurasa ramsi wa Instagram wa msanii huyo huku ikiambatana na ‘Trela’ ya filamu hiyo mbali na kusambazwa kwenye mitandao ya kutazama filamu lakini pia itaanza kuoneshwa kwenye kumbi za sinema nchini Marekani.
Filamu hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu imechezwa na Jaafar Jackson ambaye ni mpwa wa Michael Jackson, ndio ataigiza kama muhusika mkuu, huku Nia Long, Laura Harrier, Miles Teller, na Colman Domingo wakishiriki nakukamilisha orodha ya waigizaji katika filamu hiyo.
Jaafar mwenye umri wa miaka 25 ni mwanamuziki na dansa ambaye alianza kuimba rasmi akiwa na umri wa miaka 12, na alianza kujulikana zaidi mwaka 2019 baada ya kuachia wimbo wake wa ‘Got Me Singing’.
Ikumbukwe kuwa Michael Jackson alizaliwa mwaka 1958 na kufariki dunia mwaka 2009. Alitamba na nyimbo zake kama Smooth Criminal, Thriller, Will You Be There na nyinginezo.

0 Comments