Baada ya kushinda tuzo tano za Grammy mwaka jana kutokana na wimbo maarufu wa 'Not Like Us', rapa kutoka Marekani, Kendrick Lamar anaonekana kuwabeba wasanii wa Hiphop katika tuzo hizo kubwa duniani.
Kwa mujibu wa tovuti ya Gold Derby maarufu kwa kutabiri washindi wa tuzo kubwa Lamar kwa sasa anaongoza katika nafasi za ubashiri za tuzo ya Wimbo Bora wa Mwaka (Song of the Year) kupitia kolabo yake na SZA ya wimbo wa 'Luther'.
Novemba 7 mwaka huu ndipo majina ya wasanii watakaowania Grammy yatatangazwa kisha tuzo hizo zitatolewa Jumapili ya Februari 2 2026 katika Ukumbi wa Crypto.com Arena huko Los Angeles Marekani.
KUWEKA HISTORIA
Kendrick ambaye tayari ana jumla ya tuzo 22 za Grammy katika maisha yake ya muziki, amekuwa mmoja wa wasanii wachache wanaounganisha ubunifu wa kisanaa na umaarufu wa kibiashara.
Wimbo wa 'Luther' umetoka katika albamu yake ya sita, GNX na umeweka rekodi ya kukaa wiki 13 mfululizo kileleni mwa Billboard Hot 100, jambo lililofanya uzito wake kwenye kinyang'anyiro cha Grammy kuwa mkubwa zaidi kuliko hata 'Not Like Us'.
Kwa sasa Gold Derby inampa Lamar nafasi ya asilimia 95.3 ya kushinda tuzo hiyo, ikiwa ni nafasi ya juu zaidi kuliko wasanii wengine wote wanaotajwa.
WASHINDANI WENGINE
Kinyume na miaka ya nyuma rap ilitawala, mwaka huu ushindani ni mpana zaidi hasa kutoka kwa wanamuziki wa pop, soul, R&B na Amapiano.
Katika ubashiri wa Gold Derby, nafasi ya pili inashikiliwa na Sabrina Carpenter kupitia wimbo wake 'Manchild' akiwa na asilimia 91.6, huku Lady Gaga akiwa karibu na 'Abracadabra' (asilimia 91.3).
Billie Eilish, ambaye mara nyingi amekuwa kipenzi cha Grammy, yuko nafasi ya nne kupitia 'Wildflower' wakati Alex Warren msanii chipukizi ambaye amefanya vizuri mwaka huu anashikilia nafasi ya tano kupitia 'Ordinary'.
Wasanii wengine waliopo kwenye orodha ya 10 bora ni pamoja na Bad Bunny, Elton John & Brandi Carlile, Chappell Roan, Rosé, Bruno Mars pamoja na Gracie Abrams.
WIMBO WENYEWE
Wimbo wa 'Luther' ni kolabo yenye nguvu kati ya Kendrick Lamar na SZA, ikiunganisha sauti za R&B na ubeti mzito wa rap unaogusa hisia.
Wimbo huo ulitungwa na timu kubwa ya wanamuziki akiwemo Atia Boggs (Ink), Samuel Dew, Scott Bridgeway, Mark Spears (Sounwave), Jack Antonoff, Kamasi Washington, Matthew Bernard, Roshwita Bacha na kipande cha ubunifu kinachompa heshima Marvin Gaye.
Mchanganyiko huo wa sauti na ujumbe wa kijamii ndio umefanya kuonekana kama wimbo unaounganisha vizazi jambo ambalo linaonekana kupendwa na wapiga kura wa Grammy.
LADY GAGA, SABRINA
Hata hivyo njia ya Lamar si rahisi. Lady Gaga, Sabrina Carpenter na Billie Eilish wote ni majina makubwa ambayo yamekuwa yakivutia kura nyingi kutoka kwa wanachama wa Recording Academy.
Lady Gaga amerudi kwa kishindo kupitia 'Abracadabra' wimbo ulioelezewa kama mchanganyiko wa uchawi wa sauti na ujumbe wa upendo wa ndani.
Billie Eilish ambaye mara nyingi hushinda kwenye vipengele vya Record na Song of the Year, ana mashabiki wengi kwenye Academy kutokana na ubunifu wake wa kipekee.
Sabrina Carpenter licha ya kuwa chipukizi ukilinganisha na majina hayo, amekuwa gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii na majukwaa ya muziki jambo linaloongeza nafasi yake.
ΑΝΑΙΒΕΒA HIPHOP
Wakati muziki wa rap ukionekana kuporomoka kwenye chati za Billboard kwa mara ya kwanza tangu 1990 hakuna wimbo wa rap ulioingia kwenye Top 40 Lamar bado anabeba matumaini ya mashabiki wa hip-hop.
Kwa wengi ushindi mwingine wa Kendrick Lamar utakuwa ni ishara kwamba muziki wa rap bado una nafasi kubwa kisanaa hata kama haupo kileleni kibiashara.
Ikiwa 'Luther' itateuliwa kama inavyotarajiwa na labda kushinda, itakuwa ushindi mwingine kwamba Kendrick Lamar si tu rapa bora wa kizazi kipya bali pia ni msanii anayefafanua muziki wa karne ya 21.
Kama historia itajirudia, huenda Grammy 2026 ikawa tena usiku wa Kendrick Lamar mwana wa Compton ambaye kila mwaka anathibitisha kuwa sauti ya muziki wa kisasa bado iko mikononi mwake.

0 Comments