Kampuni moja kutoka China ijulikanayo kama ‘Pang Dong Lai’ imezua gumzo mitandaoni baada ya kampuni hiyo kutoa likizo maalumu kwa wafanyamazi wasio na furaha. Inasemekana kuwa mfanyakazi anayehisi hana furaha au amechoka kiakili anaweza kuomba hadi siku 10 za kupumzika bila kusumbuliwa na Bosi.
Mwanzilishi wa kampuni hiyo, Yu Donglai kwenye moja ya mahojiano yake ameeleza kuwa binadamu ana siku ambazo moyo wake unakuwa chini, hivyo hakuna sababu ya kumlazimisha mtu kufanya kazi wakati hana Amani.
“Nataka kila mfanyakazi awe na uhuru. Kila mtu ana nyakati ambazo hazifurahii, hivyo ikiwa hauko na furaha, usije kazini,”
Sera hiyo imezua mijadala mingi mitandaoni kwa sababu ni nadra kusikia kampuni inaweka ustawi wa wafanyakazi mbele kuliko masuala ya kutengeneza fedha. Wengi wameisifu kwa ubinadamu, huku wakidai kampuni nyingine nazo zifuate mfano huo.
Hata hivyo, kuna wachache wanaoona kwamba ingawa likizo hizo ni nzuri, kampuni nyingi zinapaswa kushughulikia chanzo cha msongo wa mawazo kazini badala ya kutoa tu likizo za kupumzika.

0 Comments