AZAM FC YAAJIRI CEO MSPANIOLA ALIKUWA ‘BOSI MKUBWA’ WA LA LIGA

AZAM FC YAAJIRI CEO MSPANIOLA ALIKUWA ‘BOSI MKUBWA’ WA LA LIGA

 

BODI ya Azam FC imetambulisha Mspaniola, Octavi Anoro (42) kuwa Mtendaji Mkuu (CEO) wake mpya kwa mkataba wa miaka miwili, hadi 2027.
Nafasi hiyo ilikuwa wazi kufuatia aliyekuwa akiishikilia, Abdulkarim Nurdin maarufu kama Popat, kupandishwa cheo na kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais.
Anoro, raia wa Hispania, anakuja na maarifa na uzoefu mkubwa wa kimataifa katika nyanja ya maendeleo ya utawala na biashara ya mpira wa miguu ikiwemo kuwa Mkurugenzi wa Kimataifa wa LaLiga.
Aidha, Bodi ya Azam FC, klabu inayomilikiwa na Bilionea Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na Familia yake – pia imemteua, Rashid Seif Mohamed kuwa Mtendaji Mkuu Msaidizi (Assistant CEO).
Rashid ni mhitimu wa Shahada ya Umahiri kwenye utawala wa michezo (Master’s in Sports Management) pamoja na ngazi ya pili ya ukocha kutoka chama cha soka cha England, FA.
Uteuzi huu ni muendelezo wa harakati za klabu kujipambanua kiweledi katika ukuaji wa kimkakati na kuweka alama muhimu kwenye mageuzi ya kiuongozi kwa ajili ya ustawi wa muda mrefu.

Post a Comment

0 Comments