
KIPA namba moja wa Simba SC, Mousa ‘Pin Pin’ Camara raia wa Guinea kesho anatarajiwa kusafiri kwenda nchini Morocco kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa goti.
Meneja Habari na Mawasiliiano wa klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kwamba matibabu hayo atakayofanyiwa Jumatatu ya Novemba 17 nchini Morocco kwa ujumla yatasababisha Camara awe nje kwa wiki nane hadi 10.
Camara aliumia dakika ya kwenye mchezo wa marudiano wa Raundi ya Pili Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United ya Botswana Septemba 28 mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam timu hizo zikitoka sare ya 1-1.
Simba ikafanikiwa kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1 kufuatia kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Septemba 20 Uwanja wa Taifa wa Botswana Jijini Gaborone.
Katika Raundi ya pili Simba iliitoa pia Nsingizini Hotspurs ya Eswatini kwa ushindi wan ugenini wa 3-0 Oktoba 19 Uwanja wa Taifa wa Somhlolo mjini Lobamba na sare ya bila mabao Oktkba 26 Uwanja wa Mkapa na kuingia hatua ya makundi, ambako wamepangwa Kundi D pamoja na Espérance de Tunis ya Tunisia, Petro de Luanda ya Angola na Stade Malien ya Mali.
Ni kipa mpya aliyesajiliwa kutoka JKT Tanzania, Yakoub Suleiman Ali ambaye pia ni kipa namba moja wa Tanzania kwa sasa ambaye amekuwa akidaka wakati ambao Camara amekuwa majeruhi.
0 Comments