Zerobrainer0 na Georges Kitchen, kuwania tuzo za Tiktok 2025

Zerobrainer0 na Georges Kitchen, kuwania tuzo za Tiktok 2025

 Zerobrainer0 na Georges Kitchen, kuwania tuzo za Tiktok 2025

Watengeneza maudhui wawili kutoka Tanzania, Fanuel Masamaki 'Zerobrainer0' na George Tumaini ‘George’s Kitchen’, wametajwa kuwania Tuzo za TikTok za mwaka 2025.

Tuzo hizo zinazotarajiwa kufanyika Desemba 6,2025 jijini Johannesburg, Afrika Kusini, zitahusisha wabunifu kutoka nchi mbalimbali za Afrika wanaotamba kwa ubunifu na ushawishi katika mitandao ya kijamii.

Wawili hao wamepata uteuzi katika vipengele tofauti ambapo Zerobrainer0 anawania tuzo ya ‘Sport Creator of the Year’ ikiwa ni mara yake ya pili kupata uteuzi huo. Ambapo mwaka 2024 alifanikiwa kuondoka na tuzo hiyo.

Huku kwa upande wa George akitajwa kuwania katika kipengele cha ‘Food Creator of the Year’ na hivyo kumfanya kuwa Mtanzania wa kwanza anayetengeneza maudhui ya mapishi kuteuliwa katika tuzo hizo.

George ambaye amejizolea umaarufu kufuatia na mtindo wake wa kipekee wa kupika huku akiwa amevalia kanga. Wakati akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu ameeleza kuwa hakuwa anaamini mpaka pale alipotumiwa tiketi za ndege.

“Nimekuwa Mtanzania wa pili, na wa kwanza anayetengeneza maudhui ya mapishi, kuteuliwa kwenye tuzo hizi. Baada ya kupokea tiketi ndipo nilipotambua kwamba hii ni halisi.

"Rafiki zangu walikuwa wananipigia simu, ‘Bro, uko sawa kweli?’ Lakini bado nilihisi kama si kweli. Hata hivyo, sasa ndiyo ninaamini kama kweli ninakwenda kuliwakilisha taifa langu,”amesema George

Kwa upande wa Zerobrainer0 amekuwa kivutio kwenye TikTok kwa maudhui yake ya kuchekesha yanayohusiana na soka, yaliyomfanya kujizolea maelfu ya mashabiki duniani kote.

Kwa mara nyingine, tuzo hizo za TikTok zimekuwa jukwaa la kuwapa fursa wabunifu, wasanii na watengenezaji wa maudhui, huku zikitaja mwaka 2025 kuwa mwaka ambao ubunifu umeongezeka zaidi kuliko miaka iliyopita na kuwafanya watengeneza maudhui wamekuwa na ushawishi mkubwa kwa jamii.

Post a Comment

0 Comments