
TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa kirafiki asubuhi ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Mabao ya Simba yamefungwa na mshambuliaji Mghana, Jonathan Sowah, winga Mkongo Elie Mpanzu mawili kila mmoja na winga mzawa, Ladack Chasambi na kiungo Muivory Coast, Jean Charles Ahoua.
Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa kwanza wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Petro de Luanda ya Angola Novemba 21 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
0 Comments