SIMBA SC YAKOSA TUZO YA KLABU BORA AFRIKA

SIMBA SC YAKOSA TUZO YA KLABU BORA AFRIKA

 

TIMU ya Simba SC imetupwa nje ya kinyang’anyiro cha Tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) — ikizidiwa kete na Pyramids ya Misri, RS Berkane ya Morocco na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini zilizoingia Fainali.
Simba ni kati ya timu 10 zilizoteuliwa awali kuwania Tuzo hiyo — nyingine sita ni CR Belouizdad, CS Constantine zote za Algeria, ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Orlando Pirates, Stellenbosch za Afrika Kusini na Al Hilal ya Sudan.
Tumaini la Simba sasa limebaki kwa beki Shomari Kapombe anayewania Tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika dhidi ya Ismael Belkacemi (Algeria/Al Ahli Tripoli), Blati Toure (Burkina Faso/Pyramids FC), Issoufou Dayo (Burkina Faso/RS Berkane), Fiston Mayele (DR Congo/Pyramids), Ahmed Samy (Egypt/Pyramids), Emam Ashour (Egypt/Al Ahly), Ibrahim Adel (Egypt/Pyramids), Mohamed Hrimat (Morocco/AS FAR), Mohamed Chibi (Morocco/Pyramids) na Oussama Lamlioui (Morocco/RS Berkane).
Aidha, mshambuliaji wa Yanga Clement Francis Mzize pia ameingia kwenye orodha ya awali ya Tuzo ya Bao Bora Afrika kutokana na bao lake katika ushindi wa 3-1 dhidi ya TP Mazembe Januari 4 mwaka jana kwenye mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Siku hiyo Mzize alifunga mabao mawili na linalowania Tuzo hiyo ni la kwanza alilofunga dakika ya 33 ambalo lilikuwa la kusawazisha kufuatia kipa Msenegal, Aliouane Badara Faty kuanza kuifungia TP Mazembe kwa mkwaju wa penalti dakika ya 16.
Mzize aliifungia Yanga bao la tatu pia dakika ya 60 baada ya kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki ambaye kwa sasa amehamia Wydad Athletic ya Morocco kuifungia Yanga bao la tatu dakika ya 56.

Post a Comment

0 Comments