
Kocha wa Yanga SC, Pedro Gonçalves, amemtaja fundi wa klabu ya FAR Rabat, Youssef Al Fahli, kuwa mmoja wa wachezaji ambao kikosi chake kitahitaji kuwa makini naye kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa Jumamosi hii.
Gonçalves amesema Al Fahli amekuwa na mchango mkubwa katika ubora wa FAR Rabat kutokana na kasi, ubunifu na uwezo wake wa kufanya maamuzi ndani ya eneo la hatari, hivyo wanahitaji maandalizi makubwa ili kumzuia kuleta madhara.
“Ni mchezaji mwenye ubora wa juu na anayejua kubadili aina ya mchezo muda wowote. Tutahitaji nidhamu ya juu kumzuia,” alisema Kocha Gonçalves.
Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na morali nzuri baada ya kukimbiliq Zanzibar kwa ajili ya michezo ya Ligi ya Mabingwa, huku mashabiki wakingoja kuona namna watakavyokabiliana na ubora wa Waarabu.
0 Comments