
MICHEZO:Clement Mzize atawakilishwa na Rais wa Yanga SC na M/Kiti wa ACA, Eng. Hersi Said kwenye CAF AWARDS zinazofanyika leo Rabat, Morocco, Mzize anawania tuzo ya goli bora Afrika.
Clement Mzize hajasafiri baada ya ushauri wa daktari kutokana na Upasuaji wa goti aliofanyiwa hivyo hapaswi kusafiri kwa umbali mrefu.
Clement Mzize ni mchezaji pekee kutoka Tanzania ambae amesalia hadi hatua ya mwisho kwenye tuzo za CAF ambazo leo Novemba 19, 2025 zitafanyika nchini Morocco, Rabat.
Kumbuka Eng. Hersi Said yupo nchini Morocco, Rabat katika shughuli zake kama Mwenyekiti wa chama cha Vilabu Afrika (ACA).
0 Comments