Moja ya siku ambayo hatiokuja kusahaulika na mashabiki pamoja na wadau wa muziki wa Hip Hop ni siku ambayo rapa Tupac Shakur alifariki dunia kwa kupikwa risasi. Inaelezwa kuwa Septemba 7, 1996 alikuwa Las Vegas na alitamani kwenda kushuhudia pambano la Mike Tyson dhidi ya Bruce Seldon ambapo aliongozana na aliyekuwa mfanyabiashara wa muziki Suge Knight pamoja na mpenzi wake Kidada Jones.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa familia ya Tupac walieleza kuwa Pac alikuwa mtu ambaye hakupenda kutoka bila ulinzi, na mara nyingi alivaa koti lake la kuzuia risasi kutokana na kuwa na migogoro ya muda mrefu na makundi mbalimbali ya mitaani.

Hata hivyo, siku hiyo mambo yalikuwa tofauti ambapo aliyekuwa mpenzi wake Kidada alisimulia kuwa alipokuwa akimuandaa Tupac kwenda uwanjani kuangalia pambano hilo alimfuata chumbani na kumkumbusha avae koti lake la kuzuia risasi kama ilivyokuwa desturi yake. Lakini Tupac, akiwa katika hali ya utulivu na akionesha kutokuwa na wasiwasi wowote, alimwambia kwamba hatoweza kuvaa kutokana na joto kali ‘Kuna joto sana leo’.
Baada ya pambano hilo kumalizika mapema kwa Tyson kushinda ndani ya dakika moja, kundi hilo lilitoka nje ya ukumbi wa MGM Grand ambapo kulitokea mzozo kati ya Tupac na kijana mmoja waliyehusishwa na kundi la wahalifu la Southside Crips, licha ya tukio hilo Tupac na Suge waliendelea na safari kuelekea klabu ya 662, ambako Tupac alitakiwa kutumbuiza usiku huo.
Wakati wakiwa wamesimama kusubiri taa za barabarani ziwaruhusu kuendelea na safari katika barabara ya Flamingo gari aina ya Cadillac ambalo lilikuwa na watu wasiojulikana lilisimama upande wa kulia wa gari lao na ndipo mtu aliyekaa kwenye kiti cha nyuma alianza kufyatua risasi mfululizo. Risasi hizo zilimpiga Tupac kwenye kifua, mkono na kwenye paja, huku Suge akipata majeraha madogo yaliyotokana na vioo vilivyopasuka.
Tupac alikimbizwa hospitali ya University Medical Center ambako alipelekwa chumba cha wagonjwa mahututi na baada ya siku sita za kupambana na majeraha, Tupac alifariki dunia Septemba 13, 1996.

0 Comments