
Semaji la Mnyama @ahmedally_ Ameandika ujumbe masaa machache baada ya kuibuka kwa taarifa za kiungo wa Yanga Aziz Andabwile kuda stahiki zake.
Ahmed Ally ameandika ujumbe ambao unahusishwa kulenga sakata hilo licha ya maelezo yake kutotaja jina la nyota huyo ambaye tayari ameshakanusha tetesi hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram.
“Nimeisikia Kesi ya Andambeee kuwa anaidai Nyumani Mwiko pesa ya usajili”
“Ni aibu kwa karne hii klabu kuwa na kesi kama hizo tena klabu inayojinasibu kuwa na viongozi wa kisasa”
“Huu ni muendelezo ya unyanyasi kwa Wachezaji hasa Wazawa ambao bahati mbaya wamekua waoga kudai haki zao”
“Andambeee ameamua kujivika mabomu na kuwashtaki waajiri wake asingefanya hivyo angedhulumiwa mchana kweupe”
“Kila klabu inadaiwa lakini kwanini nyinyi sana? Halafu ni kwanini Wachezaji wa Kibongo pekee iko namna mnawachukulia poa na kuwadharau”
“Kama Andambee ana muda mrefu klabuni na hajawahi kulipwa maana ake waliosajiliwa msimu huu wamekopwa na hakuna uwezekano wa kulipwa mpaka waende kushtaki”Ameandika Ahmed Ally.
0 Comments